RABA ONEFEEL FREE WITH IT

Sera

Usafirishaji, Malipo na Kurudisha Mzigo

1. Sera ya Usafirishaji na Utoaji wa Mzigo

Jijini Dar es Salaam

  • Rejareja: mzigo hufika ndani ya saa 24–48 baada ya malipo kuthibitishwa.
  • Gharama: TSh 3,000–7,000 kulingana na eneo. Bure kwa oda zaidi ya TSh 100,000.
  • Jumla: usafirishaji kwa gari la kampuni ndani ya siku 1–2; bure kwa katoni 20+.

Mikoani

  • Tunasafirisha kupitia mabasi na kampuni za usafirishaji zinazoaminika.
  • Muda: siku 2–5 kulingana na umbali wa mkoa.
  • Gharama hulipwa na mteja kulingana na uzito na mkoa; mawakala hupata viwango maalum.
  • Mteja hupewa namba ya mzigo (risiti) na hutaarifiwa kwa SMS/WhatsApp mzigo unapoondoka na kufika.

2. Sera ya Malipo

  • Mobile Money: M-Pesa, Tigo Pesa (Mixx by Yas), Airtel Money na HaloPesa.
  • Benki: uhamisho wa moja kwa moja kwenye akaunti ya kampuni (maelezo hutolewa wakati wa oda).
  • Rejareja: malipo kamili kabla ya mzigo kutumwa; Dar es Salaam pia tunakubali kulipa unapopokea.
  • Jumla: malipo ya awali ya angalau 50%, salio kabla ya mzigo kupakiwa. Mawakala waliothibitishwa wanaweza kupata masharti ya mkopo.
  • Risiti rasmi (EFD) hutolewa kwa kila malipo.

3. Sera ya Kurudisha Mzigo

  • Taarifa ya bidhaa iliyoharibika au isiyolingana na oda itolewe ndani ya saa 48 baada ya kupokea, pamoja na picha.
  • Bidhaa zirudishwe katika vifungashio vyake vya awali bila kutumika.
  • Tutabadilisha bidhaa au kurejesha fedha ndani ya siku 7 baada ya kuthibitisha tatizo.
  • Gharama za usafiri za kurudisha hulipwa na RABA ONE ikiwa kosa ni letu.
  • Bidhaa zilizotumika au kuharibika kwa uhifadhi mbaya wa mteja hazitarudishwa.